KIBALI CHA UJENZI

KIBALI CHA UJENZI (building Permit)
1.Kinatolewa na idara za upangaji mji na uhandisi ndani ya Halmashauri husika.
2.Unatakiwa kusasilisha michoro ya ujenzi ktk faili moja ambalo utaambatanisha michoro.
(a) Mwonekano wa nyumba (Elevations) mbele,nyuma pembeni na Juu
(b) Mchoro wa mfumo wa nondo (Stuctural drawings)
(c) Mchoro wa mfumo wa Umeme
(d) Mchoro wa mfumo wa maji Safi na maji taka
(e)Mchoro wa Kiwanja (Site Plan)
2.Ambatanisha kopi ya hati ya umiliki wako (Certificate of Occupancy)
i/ Kwa sehemu za Dar es Salaam Halmashauri zote zimekubalina kutoa vibali ktk maeneo ambayo hayajapimwa pia
ii/ kama eneo halijapimwa utapewa fomu kutoka Halmashauri ambazo utazisainisha ngazi ya kata,mtaa na majirani kuzunguka kiwanja chako kama wanaridhia umiliki wa Kiwanja chako.
3.Halmashauri husika itakadiria gharama za Kulipia kibali cha Ujenzi wako Kutokana na Ukubwa wa Jengo lako unalotaka kujenga na unavyo funika ardhi.
4.Halmashauri itakaa kikao cha Kamati ya Vibali vya Ujenzi na watakujibu kupitia ofisi ya Mkurugenzi, kwa Kutoa Kibali cha Ujenzi au Kama Kuna kasoro katika michoro watakutaarifu urekebishe.
5.Sheria inasema miezi 6 tangu uombe Kibali cha Ujenzi,Wasipo kujibu unaruhusiwa kujenga bila Kibali chao,na hakuna watakachokufanya.
6.Ukimaliza Ujenzi utatakiwa kurudi Halmashauri tena Kupewa Kibali cha Kuingia kwenye Jengo na Kuanza Kuishi baada ya Kukaguliwa (KIBALI CHA KUANZA KUISHI KWENYE NYUMBA)
Hiki watu weusi huwa hatunaga time nacho ila Watu weupe lazima wawe nacho ndiyo waingie ndani.