VITU NANE (8) MUHIMU VYA KUWA NAVYO ILI UWEZE KUPATA HATI MILIKI YA KIWANJA/SHAMBA
- RAMANI YA UPIMAJI
Eneo husika lazima liwe na ramani ya upimaji ambayo imeizinishwa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, iwe na mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa ramani na upimaji.
2. RAMANI YA MIPANGO MIJI
Eneo husika lazima liwe nar ramani ya mipango miji yenye kuonyesha matumizi husika ya eneo lako. Lazima iwe imeizinishwa na wizara na ina mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa mipango miji.
3. MKATABA WA UMILIKI
Lazima uwe na mkataba wa umiliki wa eneo lako, kama ulinununa, ulipewa zawadi, ulirithi n.k, Uwe na mhuri wa mwanasheria.
4. FOMU YA MIPAKA (SF 92)
Lazima uwe na fomu ya mipaka ambayo itaonyesha majirani unaopakana nao pande zote wakisaini kukubaliana na mipaka, itasainiwa pia na viongozi wa serikali yako ya mtaa.
5. FOMU YA MAOMBI YA HATI (SF. 19)
Fomu kwa ajili ya maombi ya hati, unajaza taarifa zako mfano jina, anuani,sahihi n.k
6. KITAMBULISHO CHA TAIFA Cha NIDA
7. HATI YA UTAMBULISHO (AFFIDAVIT)
8. PICHA (PASSPORT SIZE)
NB; Muhtasari unahitajika kwenye baazi ya mikoa, pamoja na hati za mashamba. Wasiliana nasi leo
@Hamiahapa (Instagram/Twitter/Facebook) au client@hamiahapa.co.tz
Podcast yetu ya kwanza inaongelea MILKI KUU (REAL ESTATE), inapatikana hapa https://audiomack.com/milkinamali